YANGA YATOSHANA NGUVU NA AZAM KWA MKAPA - Dizo Click

Dizo Click

Hot

Post Top Ad

Tuesday, 6 September 2022

YANGA YATOSHANA NGUVU NA AZAM KWA MKAPA


 

KIKOSI cha Azam FC kimeambulia pointi moja kwenye mchezo wa ligi dhidi ya Yanga wakiwa ugenini kwa mara ya kwanza ndani ya ligi.

Mechi mbili ambazo Azam ilicheza ilikuwa Uwanja wa Azam Complex iliambulia sare moja na ushindi mchezo mmoja hivyo leo inakuwa ni sare ya pili.

Azam FC Ikiwa chini ya Kali Ongala, ambaye ni kocha wa washambuliaji walianza kupachika bao la kuongoza kupitia kwa Daniel Amoah dakika ya 25 kisha Yanga wakafunga bao la kusawazisha kupitia kwa Feisal Salum dakika ya 57.

Bao la pili kwa Azam FC limefungwa na Malicous Ndoye dakika ya 65 kisha Fei dakika ya 77 akasawazisha kwa mara nyingine na kufanya ubao usome Yanga 2-2 Azam FC.

Yanga inafikisha pointi 7 kibindoni baada ya kucheza mechi tatu na sare moja na ushindi kwenye mechi mbili huku Azam FC ikifikisha pointi tano ina sare mbili na ushindi kwenye mchezo mmoja.

Katika mchezo wa leo, Yanga walikosa penalti iliyopigwa na Djuma Shaban baada ya kipa Alhamada kuiokoa.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad