SIMBA WATUNGULIWA KIMATAIFA - Dizo Click

Dizo Click

Hot

Post Top Ad

Sunday, 12 February 2023

SIMBA WATUNGULIWA KIMATAIFA


KWENYE anga anga za kimataifa kwa Simba ambao ni wawakilishi wa Tanzania katika Ligi ya Mabingwa Afrika wamekwama kupata pointi ugenini baada ya kuhushudia wakiyeyusha pointi tatu ugenini mazima katika mchezo wao wa kwanza.

Baada ya dakika 90 kukamilika kwenye mchezo wa hatua ya makundi ubao wa Uwanja wa  General Lansana Conte  umesoma Horoya 1-0 Simba.

Bao la ushindi kwa Horoya likuzana kimiani mapema dakika ya 18 na Pape Ndiaye alihusika kupeleka maumivu kwa Simba baada ya kumtungua Aishi Manula.

Mchezo huo ulikuwa na matumizi makubwa ya nguvu ndani ya Uwanja wa ulikuwa ni wa kwanza kwa timu hizo kwenye hatua ya makundi na zote zikiwa zipo kundi C.

Kuna sababu mbalimbali ambazo zimeipa ugumu Simba kuambulia angalau pointi moja ikiwa ni pamoja na wapinzani wao kuwa ni mijitu iliyokwenda hewani na inatumia nguvu mwanzo mwisho.

Hata bao la Simba walitunguliwa kwa pigo la kichwa ambalo lilimshinda Manula aliyekuwa langoni.

Sababu nyingine ni kushindwa kutengeneza nafasi nyingi kwenye mchezo huo na hata zile ambazo walitengeneza walikwama kuzitumia.

Moja ya nafasi ya dhahabu iliyotengenezwa ni ile ya dakika ya 79 ambapo nahodha John Bocco akiwa ndani ya 18 alikosa utulivu na kupiga mpira nje kidogo ya lango.

Mshambuliaji Jean Baleke ambaye alianza kikosi cha kwanza alikwama kuonyesha makeke yake kutokana na kutotengenezewa nafasi nyingi kutoka eneo la viungo washambuliaji na wakabaji.

Pia kwenye mchezo huo wakabaji wote ambao ni Mzamiru Yassin, Sadio Kanoute na Ismail Sawadogo walioanza kwa mara ya kwanza kimataifa walionekana kuwa na mpango kazi mmoja kujilinda pekee jambo lililochelewesha mashambulizi.

Aidha Kocha Mkuu wa Simba, Roberto Oliveira amesema kuwa walikuwa na uchovu kutokana na safari lakini wamecheza kwa juhudi kusaka ushindi.


Licha ya Manula kutunguliwa alifanya kazi kubwa kuokoa hatari ilikuwa dakika ya 4,8,13,14,40 kwenye kipindi cha kwanza.

Shukrani kwake pia kwa kuokoa penalti dakika ya 71 iliyosababishwa na Joash Onyango ambaye alionyeshwa kadi ya njano kwenye mchezo huo.

Utulivu wa Manula ulimpa nguvu kumsoma mpigaji Ndiaye ambaye penalti yake iligota kwenye mikono ya Manula.

 Simba ambao ni wawakilishi wa Tanzania kwenye anga la Ligi ya Mabingwa Afrika wanakibarua kingine kwenye mchezo wa pili wa dhidi ya Raja Casablanca ambapo watakuwa Uwanja wa Mkapa.

 

Mchezo huo unatarajiwa kuchezwa Februari 18 ikiwa ni mara ya kwanza ndani ya 2023 timu hiyo kucheza ikiwa nyumbani.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad