MTAMBO wa mabao ndani ya Ligi Kuu Bara, Aziz KI hajawa kwenye kikosi hicho katika mechi tatu mfululizo ambazo ni dakika 270 huku majukumu yake ya mapigo huru yakiwa kwenye miguu ya Pacome Zouzoa ambaye alikuwa na balaa.
Sababu kubwa ya Aziz mwenye mabao 10 na pasi mbili za
mabao kutokuwa kwenye mechi hizo alikuwa katika majukumu ya timu ya taifa ya
Burkina Faso ambayo ilikuwa inashiriki mashindano ya Kombe la Mataifa ya
Afrika, (AFCON).
Mchezo wa mwisho kwa Burkina Faso ilikuwa dhidi ya Mali
iliyoishia hatua ya robo fainali langoni alianza kipa Djigui Diarra ambaye naye
anacheza ndani ya Yanga.
Ni mchezo wa raundi ya pili Azam Sports Federation ilikuwa dhidi
ya Hausing FC, Uwanja wa Azam Complex Yanga iliposhinda kwa mabao 5-1 kisha
kwenye mchezo wa ligi dhidi ya Kagera Sugar 0-0 Yanga ilikuwa ni ligi na dakika
270 zilikamilika Yanga 1-0 Dodoma Jiji.
Kwenye mchezo dhidi ya Kagera Sugar Pacome alipiga faulo dakika
ya 56, 82,90 na alipiga shuti ambalo lililenga lango dakika ya 69. Mchezo dhidi
ya Dodoma Jiji, Pacome alipiga kona dakika ya 60 na alipiga shuti ambalo
lililenga lango dakika ya 60.
Hivyo mikoba ya Aziz KI ilikuwa kwenye miguu ya Pacome ambaye
alikuwa akishirikiana na wachezaji wengine wa Yanga kutimiza majukumu yao ya
kila siku uwanjani.
No comments:
Post a Comment