KIVUMBI cha msako wa bingwa mpya wa Azam Sports Federation kinaendelea ambapo katika raundi ya pili wababe walikuwa kazini kila timu kusaka ushindi.
Kagera Sugar waliibuka na ushindi wa mabao 4-0 dhidi ya Dar City
ambao wameumaliza mwendo. Katika ardhi ya Dar vigogo wawili walikuwa kazini
wakiandika rekodi namna hii:-
Hat trick hii hapa
Mwamba Clement Mzize mshambuliaji wa Yanga alifunga hat trick
kwenye mchezo wa raundi ya pili dhidi ya Hausing kwenye mchezo huo alifunga
mabao hayo kipindi cha kwanza alifunga mabao mawili na kile cha kwanza bao
moja.
Ni dakika ya 26, 32 na 35 mwamba huyo alifunga huku mfunguzi wa
bao la kwanza akiwa ni kiungo Jonas Mkude dakika ya 19 na lile la pili
lilifungwa na Skudu Makudubela dakika ya 25.
Mabao 10 yakusanywa
Ndani ya dakika 180 kwenye mechi mbili tofauti ni mabao 10
yalikusanywa raundi ya pili katika Uwanja wa Azam Complex uliotumika na vigogo
wa Dar.
Walianza mabingwa watetezi Yanga waliotwaa ubingwa wa Azam
Sports Federation kwa ushindi dhidi ya Azam FC 2023 ambapo walipata bao 1-0
lililofungwa na Kennedy Musonda Uwanja wa Mkwakwani, Tanga.
Kwenye mchezo wa Yanga ni mabao sita yalikusanywa ambapo Yanga
5-1 Hausing FC ya kutoka Njombe. Bao la Hausing lilifungwa dakika ya 69 na
nyota Tony Jailos ambaye alitoka kuwafunga Mgororo ya Mufindi mabao mawili
kwenye mchezo wao uliopita.
Mchezo wa pili ulikuwa ni Januri 31 ambapo ubao wa Uwanja wa
Azam Complex ulisoma Simba 4-0 Tembo.
Wapya kazini
Nyota Shekhan Khamis alikuwa miongoni mwa nyota waliokuwa kwenye
mchezo dhidi ya Hausing na alipiga shuti ambalo halikulenga lango dakika ya 85
huku Joseph Guede akitambulishwa kwenye mchezo huo.
Kwa upande wa Simba ni Michael Fred alianza kikosi cha kwanza na
alitoa pasi ya bao dakika ya 11 kwa Luis Miquissone, Pa Jobe alitokea benchi
alifunga bao dakika ya 83 na Saleh Karabaka naye alianzia benchi alifunga bao
dakika ya 81.
Edwin Balua na Ladack Chasambi walipata nafasi ya kuonyesha
uwezo wao kwenye mchezo huo awa funga Januari 31.
Ntibanzokiza katika ubora
Kwenye mabao manne ambayo yalifungwa na Simba Saido Ntibanzokiza
alikuwa kwenye ubora wake alipohusikakatika mabao matatu, alitoa pasi mbili za
mabao na kufunga bao moja kwenye mchezo huo.
Makipa kazini
Kipa wa Yanga, Aboutwalib Mshery alifungwa bao moja dhidi ya
Hausing ambao walipiga jumla ya mashuti mawili yaliyolenga lango huku Hussein
Abel aliyeanza langoni kwenye mchezo dhidi ya Simba yeye hakufungwa.
Kadi za njano
Nyota wawili wa Hausing walionyeshwa kadi za njano ilikuwa
dakika ya 75 Prince Anthony na dakika ya 76 Elia Lazaro huku kwenye mchezo wa
Simba dhidi ya Tembo beki Shomari Kapombe alionyeshwa kadi ya njano dakika ya
76.
Bao la mapema
Azam Complex ilishuhudia bao la mapema likifungwa dakika ya 11
na mtupiaji alikuwa ni Luis huku lile la jioni pia likifungwa na Pa Jobe dakika
ya 83.
No comments:
Post a Comment