SIMBA HAO FAINALI, MWAMBA HUYU HAPA - Dizo Click

Dizo Click

Hot

Post Top Ad

Tuesday 9 January 2024

SIMBA HAO FAINALI, MWAMBA HUYU HAPA

 


MSHAMBULIAJI wa Simba Jean Baleke kwenye kutimiza majukumu yake Mapinduzi 2024 alifunga bao pekee dakika ya 45+3 ambalo limekuwa ni ngazi kwa Simba kutiga hatua ya nusu fainali Mapinduzi 2024.

Ikumbukwe kwamba mchezo huo ulikuwa na ushindani mkubwa ambapo Jamhuri walikuwa na mbinu ya kujilinda kwenye mchezo huo dakika zote 90 wakiwa nyuma ya mpira huku wakicheza kwa nidhamu kubwa.


Ipo wazi kwamba 2023 Simba iligotea katika hatua ya makundi hivyo imevunja rekodi yao ya mwaka uliopita.

Januari 10 itakuwa nusu fainali dhidi ya Singida Fountain Gate ambapo walipokutana katika hatua ya makundi ubao ulisoma Simba 2-0 Singida Fountain Gate.

Ni Mlangege ambao ni mabingwa watetezi hawa wanakazi ya kusaka tiketi kutinga hatua ya fainali leo Januari 9 dhidi ya APR ambapo mshindi atasonga hatua ya fainali akimsubiri mshindi kati ya Singida Fountain Gate dhidi ya Simba.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad