SINGIDA FOUNTAIN GATE: TUTAIFUNGA SIMBA - Dizo Click

Dizo Click

Hot

Post Top Ad

Tuesday 9 January 2024

SINGIDA FOUNTAIN GATE: TUTAIFUNGA SIMBA


KUELEKEA kwenye mchezo wa nusu fainali ya Mapinduzi 2024 Kocha Msaidizi wa Singida Fountain Gate, Nizar Khalfan amesema wanaamini mchezo wao dhidi ya Simba hautakuwa mwepesi ila wamejipanga kuhakikisha wanapata ushindi.

Ipo wazi kuwa walipokutana kwenye mchezo wa hatua ya makundi ubao ulisoma Simba 2-0 Singida Fountain Gate hivyo wanakwenda kukutana kwa mara nyingine tena Januari 10 kwenye hatua ya nusu fainali ambapo mshindi atakata tiketi mpaka fainali.

Kocha huyo amesema: "Hata wao wanajua shughuli yetu, wakikutana na sisi huwa si mechi ya kitoto na wangeambiwa wachague kati yetu na Azam kwenye hatua hii nadhani wangechagua kukutana na Azam na siyo Singida.

Alipoulizwa kama mechi ikifikia hatua ya penati kama ilivyokuwa kwenye Ngao ya Jamii 2023 itakuwaje!? Njzar amesema:- "Kama tukitoka sare dakika 90 , basi wao watatoka kwa penati. Hatuwezi kutoa siri ya namna ambavyo tutafanya," amesema.

Ipo wazi kwamba kabla ya kuwaondoa Azam FC hatua ya robo fainali Nizar aliweka wazi kuwa watawafunga Azam FC mwisho ikawa hivyo.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad