JEMBE LA KAZI HILI HAPA LIMETAMBULISHWA SIMBA - Dizo Click

Dizo Click

Hot

Post Top Ad

Monday 15 January 2024

JEMBE LA KAZI HILI HAPA LIMETAMBULISHWA SIMBA

 


MWAMBA Pa Omar Jobe ni mnyama mwingine baada ya kutambulishwa rasmi Januari 15 2024 ikiwa ni usajili wa kuboresha kikosi hicho kilichogotea nafasi ya pili Mapinduzi 2024.

Ipo wazi kwamba Januari 13 ubao wa Uwanja wa New Amaan baada ya dakika 90 kwenye fainali ya Kombe la Mapinduzi ulisoma Mlandege 1-0 Simba.

Joseph Akandwanao aliwakanda Simba kipindi cha pili dakika ya 54 ambapo aliingia akitokea benchi. Simba walipambana dakika zote zilizobaki safu ya ushambuliaji ilikwama kupata bao.

Anakuja kuungana na Jean Baleke kwenye upande wa ushambuliaji ambapo inatajwa kwamba huenda Moses Phiri akapewa mkono wa Thank You ndani ya timu hiyo inayonolewa na Kocha Mkuu Abdelhak Benchikha.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad