MUUNGANIKO HUU YANGA NOMA WAIPOTEZA SIMBA - Dizo Click

Dizo Click

Hot

Post Top Ad

Thursday 9 November 2023

MUUNGANIKO HUU YANGA NOMA WAIPOTEZA SIMBA

 


MUUNGANO wa nyota watatu ndani ya kikosi cha Yanga ambao ni Pacome Zouzoah, Aziz KI na Maxi Nzengeli ni dawa tatu ndani ya kikosi hicho kutokana na dozi ambazo wanatoa kwa wapinzani wao.

Mastaa hao watatu wamehusika kwenye mabao 18 kati ya 26 yaliyofungwa na timu hiyo baada ya kucheza mechi 9 ambazo ni sawa na dakika 810. Idadi hiyo ya mabao inafanya muunganiko huo kuifunika Simba jumlajumla kwenye idadi ya mabao.

Ni mabao 17 Simba imetupia baada ya kucheza mechi saba na kinara wao wa kutupia ni Jean Baleke mwenye mabao sita kibindoni akifuatiwa na Moses Phiri mwenye mabao matatu.

Pacome katupia mabao manne, Aziz KI mabao 7 sawa na Nzengeli wakiwa ni chaguo la kwanza chini ya Kocha Mkuu, Miguel Gamondi.

Weka kando suala la kufunga nyota hao ni watengeneza mipango katika timu ambapo Maxi ana pasi mbili za mabao sawa na Aziz KI huku Pacome akiwa na pasi moja ya bao

Yanga ni vinara wa ligi wakiwa na pointi 24 Novemba 8 2023 walishuhudia ubao wa Uwanja wa Mkwakwani, Tanga ukisoma Coastal Union 0-1 Yanga bao pekee la Clement Mzize aliyefunga kwenye mchezo huo ambao ulikuwa na matumizi mengi ya nguvu..

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad