SIMBA YATAMBIA KOCHA WAO MPYA - Dizo Click

Dizo Click

Hot

Post Top Ad

Wednesday 8 November 2023

SIMBA YATAMBIA KOCHA WAO MPYA


 

AHMED Ally, Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano ndani ya kikosi cha Simba amesema kwa sasa kikosi hicho kipo kwa kocha mwenye leseni ya juu kabisa kwa muda.

Ikumbukwe kwamba Roberto Oliveira aliyekuwa kocha mkuu wa Simba amekutana na thank you baada ya kupoteza mchezo mmoja dhidi ya watani zake wa jadi Yanga.

Novemba 5 2023 ubao wa Uwanja wa Mkapa ulisoma Simba 1-5 Yanga ukiwa ni mchezo wa kwanza kupoteza pointi tatu msimu wa 2023/24 na kichapo kikubwa kuliko.

Ally amesema: "Kocha Daniel Cadena ambae amekabidhiwa jukumu la kuingoza timu yetu kwa kipindi hiki ni Kocha mwenye wasifu na uwezo mkubwa akimiliki leseni ya juu kabisa ya mpira wa miguu UEFA A LICENCE.

"Kwa sasa kikosi kipo kwenye mikono salama, Wanasimba tuendelee kuwa pamoja kwa ajili ya kupata matokeo kwenye mechi zinazofuata kazi bado inaendelea,".

Mchezo ujao kwa Simba ni dhidi ya Namungo unatarajiwa kuchezwa Novemba 9.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad