MASTAA YANGA WAPEWA KAZI NYINGINE NA GAMONDI - Dizo Click

Dizo Click

Hot

Post Top Ad

Friday 10 November 2023

MASTAA YANGA WAPEWA KAZI NYINGINE NA GAMONDI

 


MCHORA ramani za ushindi ndani ya kikosi cha Yanga, Miguel Gamondi amewapa majukumu mengine mastaa wake wakiongozwa na muunganiko wake wa PAM unaowajumuisha Pacome Zouzoah, Aziz KI na Maxi Nzengeli kuendeleza kasi yao.

Ikumbukwe kwamba PAM imehusika kwenye mabao ya kufunga 18 ambapo Pacome ana mabao manne huku Aziz KI na Maxi hawa wakiwa wametupia mabao sabasaba kila mmoja.

 Gamondi amesema kuwa jukumu la wachezaji wote ni kufanya kazi kwa ushirikiano na kuwa na kiu ya kupata ushindi kwenye kila mchezo ambao wanacheza.

“Ukianza na viungo waliopo ndani ya timu kuanzia Maxi, Aziz hawa wote ni muhimu kushirikiana kupata matokeo kwenye mechi ambazo tunacheza na hilo linawezekana kwa kuwa kila mmoja anafurahia anachokifanya.

“Tunapenda kuona namna ambavyo Pacome anafanya kazi kwa ushirikiano na wachezaji wengine kwani hili ni jukuumu la kila mchezaji. Tunacheza kupata matokoe na hilo linaonekana hivyo mashabiki wazidi kuwa pamoja nasi,” amesema Gamondi.

Yanga ni vinara wa ligi wakiwa na pointi 24 baada ya kucheza mechi 9 pointi zao kibindoni ni 24 nafasi ya pili ni Azam FC yenye pointi 19.

 


No comments:

Post a Comment

Post Top Ad