MWAMBA WA AZAM ANAFIKIRIA KUFUNGA - Dizo Click

Dizo Click

Hot

Post Top Ad

Sunday 7 January 2024

MWAMBA WA AZAM ANAFIKIRIA KUFUNGA

 


MWILI jumba ndani  ya Azam FC, Allasane Diao ameweka wazi kuwa anafikiria kuendelea kufunga kwenye kila mechi ambazo atapewa nafasi kwa kuwa ni kitu ambacho anakipenda kwa manufaa ya timu.

Nyota huyo anaingia kwenye rekodi ya kuwa mfungaji wa bao la kwanza kwa Azam FC kwenye Mapinduzi 2024 ambapo alifunga bao pekee la ushindi katika mchezo dhidi ya Chipukizi.

Mchezo huo uliochezwa Uwanja wa Amaan ilikuwa ni Desemba 30 2023 baada ya dakika 90 ubao ulisoma Chipukizi 0-1 Azam FC na bao lilipachikwa dakika ya 12.

Diao mwenye umbo la miramba minne ameweka wazi kuwa furaha kubwa ni kuona anaendelea kufunga katika mechi ambazo wanacheza.

“Ninapopata nafasi ya kucheza na kufunga hilo ninamshukuru Mungu kwa kuwa hicho ni kitu kikubwa kwangu na timu ninapenda kuona hali hii inaendelea kwenye mechi zote ambazo tunacheza,”.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad