CONTE AANZA KWA SARE HUKO - Dizo Click

Dizo Click

Hot

Post Top Ad

Wednesday, 10 November 2021

CONTE AANZA KWA SARE HUKO

 


Antonio Conte, Kocha Mkuu ea Tottenham amesema kuwa vijana wake wanahitaji muda zaidi kuweza kurejea kwenye ubora na kuonyesha kile ambacho wanacho ndani ya uwanja.


Mrithi huyo wa mikoba ya Nuno Espirito ambaye alifutwa kazi ndani ya timu hiyo kutokana na mwendo mbovu wa timu hiyo ndani ya Ligi Kuu England. 


Katika mchezo wake wa kwanza katika Ligi Kuu England,  Conte alilazimisha sare ya bila kufungana mbele ya Everton na kufanya timu hiyo ifikishe jumla ya mechi tatu mfululizo bila kushinda pia katika mchezo huo alishuhudia mchezajinwa Everton,  Mason Holgate akionyeshwa kadi nyekundu dakika ya 90+2.


Kocha huyo ameweka wazi kwamba kwa namna ambavyo ameanza na alivyowaona wachezaji hao anaamini kwamba watafanya mambo makubwa hapo baadaye. 

Mchezo wake wa pili itakuwa ni Novemba 21 ambapo atakuwa na kibarua cha kusaka pointi tatu mbele ya Leeds United. 

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad