GERRAD ATAJWA KUWA MRITHI WA KOCHA ASTON VILLA - Dizo Click

Dizo Click

Hot

Post Top Ad

Thursday, 11 November 2021

GERRAD ATAJWA KUWA MRITHI WA KOCHA ASTON VILLA



STEVEN Gerrad Kocha Mkuu wa Rangers inaelezwa kuwa ameanza mazungumzo na timu moja inayoshiriki Ligi Kuu England ambayo ni Aston Villa ili kuwa mmoja ya watakaochukua mikoba ya Dean Smith aliyefukuzwa ndani ya kikosi hicho baada ya timu hiyo kupoteza kwa kufungwa bao 1-0 dhidi ya Southampton.

Villa kwa sasa ipo chimbo kusaka kocha mpya bada ya kumchimbisha Smith siku ya Jumapili kutokana na mwendo mbovu ndani ya timu hiyo kwenye mechi za Ligi Kuu England kwa kuwa ilipoteza katika mechi tano na ipo nafasi ya 16 kwenye msimamo.

Orodha ni ndefu ya majina ambayo yanatajwa kuwa kwenye mpango wa kuibukia hapo huku jitihada za timu hiyo ikiwa ni kumpata kocha mpya mapema sana ndani ya saa 24 ama 48 zijazo ili aweze kuanza kazi hapo.

Kwa mujibu wa Sky Sports wameripoti kwamba Gerrad ambaye alikuwa anahusishwa pia kujiunga na Newcastel United na Roberto Martinez Kocha Mkuu wa timu ya taifa ya Ubelgiji ni kati ya wale ambao wanapewa nafasi kubwa ya kuwa ndani ya Aston Villa kwa wakati huu hivyo ni jambo la kusubiri na kuona nani atakuwa nani.



No comments:

Post a Comment

Post Top Ad