WANANCHI HAWANA JAMBO DOGO NI KUSHINDA TU - Dizo Click

Dizo Click

Hot

Post Top Ad

Saturday, 13 November 2021

WANANCHI HAWANA JAMBO DOGO NI KUSHINDA TU

 


WANANCHI wameendelea kuwa na furaha baada ya kushinda mabao 2-1 mbele ya KMKM FC katika mchezo wa kirafiki uliochezwa Uwanja wa Amaan, Zanzibar.


 KMKM FC walikuwa wa kwanza kupachika bao kupitia kwa Optatus Lupekenya ambaye alitumia mpira wa makosa ya Abdallah Shaibu,'Ninja kisha Lupekenya akawatungua Yanga katika mchezo uliokuwa na ushindani mkubwa.


Jesus Moloko alisawazisha bao dakika ya 27 akitumia pasi ya Deus Kaseke aliyoitoa kwa mguu wa kulia akiwa nje ya 18 huku Moloko akiwa ndani ya 18 na kupachika bao hilo kwa kichwa kilichomshinda kipa Nassoro Abdallah Nassoro.


Chuma cha pili ilikuwa kazi ya Fiston Mayele dakika ya 85 kwa pasi ya Yannic Bangala ambapi alipachika bao kwa mtindo wa kubinuka,tikitaka safi baada ya Moloko kupiga kona ya moja kwa moja katika mchezo huo wa kirafiki.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad