WAKATI vinara wa Ligi Kuu Tanzania Bara wakiwa kwenye maandalizi ya mwisho kuelekea mchezo wao dhidi ya Namungo unaotarajiwa kuchezwa kesho, Uwanja wa Ilulu, kiungo wake wa kazi Khalid Aucho atakosekana kwenye mchezo huo.
Awali ilikuwa inatajwa kuwa nyota huyo anaidai Yanga jambo ambalo limefanya aweze kugoma.
Taarifa rasmi iliyotolewa na Ofisa Habari wa Yanga,Haji Manara imeainisha kuwa nyota uyo haidai Yanga bali ni maumivu ambayo alikuwa ameyapata baada ya kupata mchubuko kwenye mguu alipokuwa kwenye timu ya taifa ya Uganda.
Manara ameweka wazi kwamba kila kitu kinakwenda sawa ila Aucho ataukosa mchezo huo kwa kuwa hawezi kucheza kwa maumivu ambayo ameyapata.
"Hakuna ambaye anaweza kucheza akiwa kwenye hali kama hiyo ila kikubwa ni kuona kwamba anarejea kwenye hali yake ya kawaida. Watu wameanza kusema kwamba Aucho anaidai Yanga hatupo kwenye hali hiyo kwa sasa kwa sababu Yanga ni timu kubwa.
"Kwanza kudaiwa ni sifa ya Taasisi yoyote imara but, (lakini) Yanga kudaiwa na mchezaji tushavuka huko, Yanga hii ya GSM kudaiwa na mchezaji ni dhambi kuu.
"Aucho alichubuka akiwa katika majukumu ya team ya taifa na katika hali hiyo aliyonayo vp angeweza kushiriki katika mehi ya kesho? "

No comments:
Post a Comment