RIPOTI YA PABLO KUHUSU USAJILI MIKONONI MWA MABOSI SIMBA - Dizo Click

Dizo Click

Hot

Post Top Ad

Monday, 27 December 2021

RIPOTI YA PABLO KUHUSU USAJILI MIKONONI MWA MABOSI SIMBA


 KAZI imeanza huko Simba kufuatia kocha mkuu wa timu hiyo, Pablo Franco kukabidhi rasmi ripoti ya usajili wa majembe mapya katika dirisha dogo lililofunguliwa Desemba 16, mwaka huu na kutarajiwa kufungwa Januari 15, 2022.

 

Baada ya kukabidhi ripoti hiyo huku akitaja wachezaji anaowahitaji,Bodi ya Wakurugenzi ya Simba itakutana katika kikao kizito kuijadili ripoti hiyo.

 

Hadi sasa, Simba inahusishwa na usajili wa wachezaji wengi wakiwemo nyota wawili raia wa Zambia Clatous Chama anayecheza RS Berkane na Moses Phiri wa Zanaco.


Kuhusiana na ishu ya usajili, kocha Pablo amesema: “Tayari nimewasilisha mapendekezo ya usajili kwa viongozi, ni kweli kuna maeneo ambayo tunahitaji kuyafanyia maboresho ili kuwa na kikosi bora zaidi.


“Siwezi kuyaweka wazi 
mapendekezo hayo kwa kuwa ni siri ya klabu, lakini jambo muhimu ni
kuwa viongozi wameanza kulifanyia 
kazi hilo.”

 

Naye Mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi wa Simba, Crescentius Magori, alisema: “Kuhusiana na usajili wa nyota wapya kwenye dirisha hili la usajili tulikuwa tunasubiri ripoti ya Kocha Pablo ili kuanza kuifanyia kazi,".

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad