YANGA YAFUNGA MWAKA KIBABE - Dizo Click

Dizo Click

Hot

Post Top Ad

Friday, 31 December 2021

YANGA YAFUNGA MWAKA KIBABE

 


DAKIKA 90, Uwanja wa Mkapa zimekamilika huku kikosi hicho kikiweza kufunga mwaka 2021 kwa ushindi wa mabao 4-0 dhidi ya Dodoma Jiji.

Kwenye mchezo wa leo ambao ulianza kwa kasi ni mabao ya Fiston Mayele dakika ya 41 kisha Jesus Moloko alipachika bao la pili dk 56, huku Justin Bilaly akijifunga dk 70 kwa pasi ya Feisal Salum.

Msumari wa kufungia mwaka 2021 kwa Yanga ulijazwa kimiani na kiungo wa kazi Khalid Aucho dk 81.

Yanga inafikisha pointi 29 inafunga 2022 ikiwa ni namba moja kwenye msimamo wa ligi msimu wa 2021/22.

Pia nyota wake wapya ambao ni Sure Boy na Aboutwalib Mshery walianza kikosi cha kwanza.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad