HUYU HAPA KOCHA MPYA AZAM FC - Dizo Click

Dizo Click

Hot

Post Top Ad

Sunday, 30 January 2022

HUYU HAPA KOCHA MPYA AZAM FC


KLABU ya Azam FC imeingia mkataba wa miaka mitatu na Omar Abdikarim Nasser, kuwa Kocha Msaidizi mpya wa timu hiyo inayoshiriki Ligi Kuu Bara.


Ujio wa Nasser aliyesaini mkataba Januari 29,2022 mbele ya Ofisa Mtendaji Mkuu, Abdulkarim Amin 'Popat', ni sehemu ya mapendekezo ya Kocha Mkuu, Abdihamid Moallin ambaye naye amesaini mkataba mpya hivi karibuni.

Nasser amewahi kufanya kazi katika nchi mbalimbali, mara ya mwisho 2019, akiitumikia moja ya vigogo vya nchini Qatar, Al Sadd, akiwa kama mchambuzi wa mechi (analyst) wa timu ya vijana chini ya umri wa miaka 23 (U-23), kabla ya kufanya majukumu kama hayo akiwa Al Duhail ya huko pia.

Al Sadd ni moja ya timu kubwa nchini humo, iliyokuwa ikinolewa na gwiji wa zamani wa Hispania, Xavi Hernandez, kabla kurejea Barcelona, akiwa kama Kocha Mkuu.

Omary, mzaliwa wa Somalia aliyekulia England na kuchukua uraia wa huko, pia alikuwa Kocha Msaidizi wa timu ya Taifa ya Somalia kuanzia mwaka jana hadi sasa.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad