KIBWANA,NINJA WAELEKEA TUNISSIA - Dizo Click

Dizo Click

Hot

Post Top Ad

Wednesday, 12 January 2022

KIBWANA,NINJA WAELEKEA TUNISSIA

 ABDALAH Shaibu beki wa kati wa Yanga ameelekea Tunissia kwa ajili ya matibabu zaidi ya maumivu ya goti ambayo alikuwa nayo kwa muda mrefu.



Pia nyota mwingine ni Kibwana Shomari beki wa kazi chafu ambaye yeye aliumia katika mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Simba.


Kocha Mkuu wa Yanga, Nasreddine Nabi hivi karibuni aliweka wazi kuwa anahitaji kuona wachezaji hao wakipelekwa Tunisia ili kupata matibabu zaidi.


"Nahitaji kuona kwamba Ninja na Kibwana wanakwenda Tunissia kama ilivyokuwa kwa Yacouba Songne ili wapate matibabu zaidi warudi kazini,".


Tayari nyota hao wameelekea huko kupata matibabu, kila la kheri.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad