MAYELE ATUPIA MBELE YA MBAO FC - Dizo Click

Dizo Click

Hot

Post Top Ad

Saturday, 29 January 2022

MAYELE ATUPIA MBELE YA MBAO FC

 


NYOTA Fiston Mayele wa Yanga kipindi cha pili ameweza kupachika bao la ushindi katika mchezo wa Kombe la Shirikisho uliochezwa Uwanja wa CCM Kirumba.


Bao hilo la Mayele lilipachikwa dakika ya 53 akiwa ndani ya 18 na kuwafanya mashabiki wa Yanga kunyanyuka jukwaani baada ya kuifunga Mbao FC.


Ushindi huo unaifanya Yanga kutimga hatua ya 16 bora baada ya ushindi katika hatua ya 32 bora.


Hamis Kasanga beki wa Mbao amesema kuwa wamepoteza kutokana na makosa ambayo waliyafanya.


Kwa upande wa Yanga, nahodha Bakari Mwamnyeto amesema kuwa walifuata maelekezo ya mwalimu na kuweza kupata ushindi.


Jumla walipiga kona 11 na Mbao walipiga kona 1 na mashuti 12 ya Yanga hayakulenga lango na ni mashuti mawili kwa Mbao yalilenga lango.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad