MUKOKO Tonombe kiungo wa Yanga leo Januari 19 ameweza kutupia mabao mawili katika mchezo wa kirafiki dhidi ya Mbuni FC.
Mchezo wa leo ulikuwa ni maalumu kwa ajili ya kutesti mitambo na nyota wapya wa Yanga pia wameweza kutumika na Kocha Mkuu, Nasreddine Nabi.
Ni dakika ya 56 na 82 Mukoko aliweza kutupia mabao hayo akitumia mguu wa kulia kwa utulivu akiwa ndani ya 18.
Mbuni FC walikuwa wakicheza mchezo wa kiume ambapo waliweza kucheza faulo nyingi na moja ni ile aliyochezewa David Bryson dakika ya 36 na Ilisababisha nyota wa Mbuni kutolewa kwa kadi nyekundu ya moja kwa moja.
Ni Hussein Idd ambaye alitolewa kwenye mchezo huo.
No comments:
Post a Comment