KIKOSI cha Simba kimetwaa Kombe la Mapinduzi kwa mara ya nne baada ya ushindi wa bao 1-0 mbele ya Azam FC yenye mataji matano.
Bao la ushindi limefungwa na Meddie Kagere kwa penalti dakika ya 55 iliyosababishwa na kipa Mathias Kigonya baada ya kuonekana akimchezea faulo Sakho.
Kagere pia ametwaa tuzo ya mfungaji bora ambapo ni mabao mawili amefunga katika Kombe la Mapinduzi sawa na Ousmane Sakho.
Nyota mwingine wa Azam FC ni Idris Mbombo ambaye naye alitupia jumla ya mabao mawili.
Ushindi wa leo unaifanya Simba kufuta uteja mbele ya Azam FC kwa kuwa kwenye fainali tatu ambazo walikutana Azam FC ilishinda na leo imepoteza katika fainali ya nne.
No comments:
Post a Comment