SIMBA YATINGA HATUA YA 16 BORA - Dizo Click

Dizo Click

Hot

Post Top Ad

Sunday, 30 January 2022

SIMBA YATINGA HATUA YA 16 BORA

 


MABINGWA watetezi wa Kombe la Shirikisho, Simba leo Januari 30 wamefanikiwa kutinga hatua ya 16 bora kwenye kombe hilo baada ya kupata ushindi wa mabao 6-0 dhidi ya Dar City.

Mchezo huo umechezwa Uwanja wa Mkapa na mabao ya Simba yalijazwa kimiani na Meddie Kagere ambaye alicheka na nyavu mara mbili na Rally Bwalya pamoja na Clatous Chama walifunga bao mojamoja kipindi cha kwanza.

Kipindi cha pili Simba ilitupia mabao mawili kupitia kwa Pascal Wawa ambaye ni beki na Chris Mugalu ambaye ni mshambuliaji na wote walikuwa wameanza benchi wakisoma mchezo.

Seleman Matola, Kocha Msaidizi wa Simba alikuwa kwenye benchi la ufundi kwenye mchezo wa leo kwa sababu Kocha Mkuu, Pablo Franco amefungiwa mechi tatu na Bodi ya Ligi Tanzania.

Ushindi huo unaifanya Simba kuweza kutinga hatua ya 16 bora na watakutana na Ruvu Shooting kwenye hatua hiyo.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad