SURE BOY,NKANE KUIKOSA AZAM FC KESHO KOMBE LA MAPINDUZI - Dizo Click

Dizo Click

Hot

Post Top Ad

Sunday, 9 January 2022

SURE BOY,NKANE KUIKOSA AZAM FC KESHO KOMBE LA MAPINDUZI

 


KUELEKEA katika mchezo wa Kombe la Mapinduzi kesho Januari 10 kati ya Yanga dhidi ya Azam FC baadhi ya nyota wanatarajiwa kuukosa mchezo huo kutokana na sababu mbalimbali.


Yanga ni mabingwa watetezi wa Kombe la Mapinduzi ambapo waliweza kulitwaa taji hilo kwa ushindi wa penalti mbele ya Simba.


Ni Salum Aboubakhari, 'SureBoy' ambaye ni kiungo na jezi yake ni namba 18 huyu anatarajiwa kuukosa mchezo. 


Sababu ya Sure Boy kuukosa mchezo ni kuugua Malaria ambayo haikubaliki.


Pia Dennis Nkane naye anatarajiwa kuukosa mchezo kwa kuwa aliumia kwenye mchezo dhidi ya KMKM kwenye sare ya kufungana mabao 2-2.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad