LEO Jumapili michuano ya AFCON 2021 inatarajiwa kufika tamati baadabya kuchezwa kwa siku 28 kuanzia Januari 8,2022.
Timu 24 zilianza hatua ya makundi hadi leo zimebaki mbili ambazo zitacheza fainali kusaka bingwa.
Ni fainali kati ya Misri yenye Mohamed Salah dhidi ya Senegal yenye Sadio Mane ambao wote wapo ndani ya Liverpool inayoshiriki Ligi Kuu England.
Salah ni kinara wa utupiaji kwa Misri akiwa ametupia mabao mawili huku Mane akiwa ametupia mabao matatu.
Mpaka inatinga fainali Senegal imefunga mabao tisa na kuruhusu mabao mawili huku Misri ikiwa imeruhusu bao moja kwa muda wa kawaida na ikifunga mabao manne.
No comments:
Post a Comment