IMEELEZWA kuwa kiungo wa Yanga, Bernard Morrison yupo kwenye hesabu za kujiunga na mabosi wake wa zamani Yanga baada ya kuzinguana na mabosi wake wa sasa ambao ni Simba.
Kwa sasa kiungo huyo amesimamishwa kwa muda usiojulikana na mabosi wa Simba kupitia taarifa rasmi ambayo imetolewa na Simba na imemtaka aweze kuandika barua ya kujieleza na akishindwa hatua zaidi zitachukuliwa.
Morrison alijiunga na Simba akitokea Yanga na hata kujiunga kwake pia kulikuwa kuna misukosuko kibao kwa kuwa hakuwa na maelewano mazuri na mabosi wa Yanga ambao walikuwa wanaeleza kwamba alikuwa na mkataba wa miaka miwili lakini mchezaji huyo aligomea kwa kueleza kuwa mkataba wake ulikuwa ni wa miezi sita.
Mkataba wake unakaribia kufika ukingoni pale msimu wa 2021/22 utakapoisha jambo ambalo linamaanisha kwamba anaweza kujiunga na Yanga bure kuendelea kuitumikia timu hiyo.
Hakuwa sehemu ya mchezo wa jana mbele ya Mbeya Kwanza wakati Simba ikishinda kwa bao 1-0 lililofungwa na Clatous Chama ambaye alifunga dakika ya 85.
No comments:
Post a Comment