SENEGAL NI MABINGWA WA AFCON 2021 - Dizo Click

Dizo Click

Hot

Post Top Ad

Monday, 7 February 2022

SENEGAL NI MABINGWA WA AFCON 2021

 


TAIFA la Senegal kwa sasa ni furaha na shwangwe za kutosha baada ya timu ya taifa kusepa na Kombe la Afcon 2021 kwa ushindi mbele ya Misri kwenye mchezo uliokuwa na ushindi mwanzo mwisho.

Ni ushindi wa penalti 4-2 walipata Senegal mbele ya Misri ambao walikuwa wakipambana kuhitaji kusepa na taji hilo kubwa Afrika nchini Camerooon.

Ni Sadio Mane ambaye alikosa penalti kipindi cha kwanza dakika ya pili baada ya pigo lake kuokolewa na kipa wa Misiri na Mane ndiye ambaye alipewa apige penalti ya mwisho iliyojaa kimiani.

Ilibidi bingwa apatikane kwa penalti kwa sababu katika dakika 90 za awali milango ilikuwa migumu na hata zilipoogezwa dakika 30 na kukamilisha dakika 120 bado hakukuwa na mshindi.

Hivyo kwa sasa mabingwa wapya ni Senegal ambao walikuwa kwenye ubora mwanzo mwisho wakikosa umakini mbele ya Misiri ambao walikuwa katika ubora kwenye fainali iliyochezwa usiku wa kuamkia leo

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad