WACHEZAJI YANGA WALICHEZA MECHI WAKIWA WAGONJWA,WAFUNGUKIA ISHU YA WAAMUZI - Dizo Click

Dizo Click

Hot

Post Top Ad

Tuesday, 8 February 2022

WACHEZAJI YANGA WALICHEZA MECHI WAKIWA WAGONJWA,WAFUNGUKIA ISHU YA WAAMUZI


UONGOZI wa Yanga umebainisha kwamba kuna mechi ambayo wachezaji wao walicheza mechi ya ligi wakiwa wanaumwa na walikataliwa kupeleka mbele mchezo wao.

Ofisa Habari wa Yanga, Haji Manara amesema kuwa katika mchezo wao wa ligi dhidi ya Tanzania Prisons walicheza wakiwa wanaumwa na wakati hayo yakitokea Simba hawakucheza mbele ya Kagera Sugar kwa kuwa wachezaji walikuwa wanaumwa.

Manara amesema: "Mechi yetu dhidi ya Tanzania Prisons ilikuwa ngumu kuliko mechi yoyote ambayo tumecheza na wachezaji walikuwa wanacheza huku wakiwa wanaumwa, Bakari Mwamnyeto alimeza panado na wachezaji muda wa mapumziko walikunywa panado sitasita.

"Hili lilitokea kwa kuwa hatukuwa na namna na hata tulipoomba mechi yetu isichezwe tuliambiwa kwamba tumechelewa kuomba na hatujafuata utaratibu hivyo tukawaambia wachezaji wetu chezeni hii mechi.

Kuhusu mwendo wa ligi hasa kwa upande wa waamuzi Manara amesema:-"Maamuzi yawe sawa anayekosea aadhibiwe,wajibu wetu sisi ni kukumbusha hatulalamiki,hatuwezi kukubali kuona haki haitendeki alafu nikae kimya,tunataka haki itendeke, " amesema.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad