HAWAAMINI macho yao imefika ukingoni kwa mashabiki wa Simba nao kutoamini walichokiona kwa wachezaji wao kushindwa kufikia lengo la kutinga hatua ya nusu fainali.
Kupoteza kwa
kufungwa penalti 4-3 mbele ya Orlando Pirates kumezima matarajio ya Simba
inayonolewa na Kocha Mkuu, Pablo Franco kutinga hatua ya nusu fainali kwenye
Kombe la Shirikisho Afrika.
Hesabu
zilikuwa ngumu ila kuna jambo la kujifunza kwa wakati ujao kwa wawakilishi wa
kimataifa namna hii:-
Matumizi ya uwanja wa nyumbani
Kweli
wametolewa lakini wamepata somo lingine kwa namna soka la Afrika lilivyo kwenye
matumizi ya uwanja wa nyumbani.
Imeripotiwa
kwamba viongozi wa Simba ikiwa ni pamoja na Mtendaji Mkuu, Barbara Gonzalez
waliweza kuzuiwa mwanzo.
Licha ya
uchache wa mashabiki wa Orlando Pirates bado walikuwa na fujo mwanzo
mwisho.Hapo kuna jambo wawakilishi wetu kimataifa Simba wanapaswa kujifunza.Kama
wangemaliza mchezo Uwanja wa Mkapa kwa kushinda mabao zaidi ya mawili ingekuwa
ni habari nyingine.
Manula jezi yake iwekwe makumbusho
Hamna namna
licha ya kufungwa bao moja kwenye mchezo wa juzi, bado Aishi Manula aliweza
kutimiza majukumu yake kwa kuliweka lango la Simba salama.
Aliweza
kuokoa mashuti manne kati ya matano ambayo yalilenga langoni huku moja likiweza
kuzama mazima kwenye nyavu zake ilikuwa kupitia kwa Kwame Peprah dk ya 60 kwa
kichwa.
Kwenye
mikwaju ya penalti, Manula hakuwa na chaguo zaidi ya kuishia kuokoa penalti
moja lakini aliweza kutimiza majukumu yake na alionyeshwa kadi moja ya njano
katika dk 90 ambazo aliyeyusha.
Hakuna shuti lililolenga lango
Mbinu kubwa
ya Simba ilikuwa ni kujilinda jamo lililofanya muziki utumie mabeki kwa
asilimia kubwa ikiwa ni pamoja na Henock Inonga, Pascal Wawa,Joash
Onyango,Shomary Kapombe,Israel Mwenda na Mohamed Hussein.
Ubunifu eneo
la kiungo ulikosekana na mshambuliaji aliyeanza Chris Mugalu aliendelea na
makosa kama mechi iliyopita Uwanja wa Mkapa kwa kucheza faulo mwisho
alionyeshwa kadi mbili za njano na kutolewa kwa kadi nyekundu.
Mpaka anatoka
alikuwa hajapiga shuti hata moja ambalo lilikuwa limelenga lango na kuwaacha
wachezaji wenzake dk ya 59 wakipambana.
Mipira iliyokufa imewagharimu
Wakiwa
pungufu licha ya kufungwa bao moja waliweza kukomaa nalo mpaka mwisho ila
kipengele cha mipira iliyokufa, (penalti) kiliwagharimu Simba kwa kuwa bahati
haikuwa yao.
Mpigaji wa
kwanza, Jonas Mkude pigo lake liliokolewa na kipa kisha Shomari Kapombe aliweza
kufunga huku Henock Inonga yeye aligongesha mwamba na kuwapa nguvu wapinzani
wao Orlando Pirates.
Ni Meddie
Kagere na Mohamed Hussein hawa penalti zao zilizama nyavuni huku Orlando wao
wakifunga penalti 4 na kuifungashia virago Simba ambao walipata penalti 3.
VAR kama VAR
Mfumo wa VAR
ulikuwa ni pasua kichwa juzi kwa kuwa uliweza kutumika na kuipa ugumu Simba
kupenya kwanza kadi ya njano ya pili kwa Mugalu iliweza kuamuriwa kwa VAR kwa
kuwa mwamuzi alikuwa hajaona.
Bao
walilofungwa Simba ilionekana kwamba ni mtego wa kuotea lakini hakukuwa na
mrejeo wa VAR na dakika za lala salama beki wa Simba, Shomari Kapombe
alionekana ameugusa mpira akiwa ndani ya 18 ila mwamuzi wa kati hakuenda
kuitazama VAR ngoma ikaendelea.
Simba kimataifa wanaishi ulimwengu
wao
Wachezaji wa
Simba inapofika kwenye hatua ya kimataifa wamekuwa wakiishi kwenye ulimwengu
wao wenyewe kutokana na kucheza kwa kujitoa na kufika hatua ya robo fainali
katika hilo wanahitaji pongezi.
Tutaonana
baadaye
Bado baadaye
tunaweza kuona tena Simba ikafanya kazi yake kwenye hatua za kimataifa kwa kuwa
bado wanashiriki Kombe la Shirikisho wakiwa hatua ya robo fainali na wapo
kwenye ligi wakiwa nafasi ya pili.

No comments:
Post a Comment