YANGA V SIMBA,HAYA HAPA MAJEMBE YA KAZI - Dizo Click

Dizo Click

Hot

Post Top Ad

Thursday, 21 April 2022

YANGA V SIMBA,HAYA HAPA MAJEMBE YA KAZI


MAKOCHA wote wawili kwa sasa wanapiga hesabu mara mbilimbili, mechi zao wanazocheza huku wakifikiria na mchezo wa Kariakoo,Dabi Aprili 30.

Ni siku 9 zimebaki kabla ya mchezo huo, hapa tunakuletea baadhi ya nyota wa kazi kwa Nasreddine Nabi wa Yanga na Pablo Franco wa Simba namna hii:-

Diarra Djigui

Kipa namba moja wa Yanga ameanza kikosi cha kwanza mechi 15 na amesepa na dk 1,350 na amefungwa mabao 5 na kakusanya clean sheet kwenye mechi 10.

Katika mabao hayo ambayo amefungwa hakuna bao alilofungwa kwa mkwaju wa penalti na lile la kwanza alifungwa na Ruvu Shooting, Uwanja wa Mkapa mtupiaji akiwa ni Shaban Msala.

Dickson Job

Job kama lilivyo jina lake yale yaliyomo yamo ni mtu wa kazi kwelikweli akiwa amecheza mechi 16 na kutumia dk 1,509 na ana pasi moja ya bao aliyotoa ndani ya ligi.

Yanick Bangala

Beki wa kazi ngumu na zile nyepsi akiwa ana uwezo wa kupanda na kushuka ametumia dk 1,431 na ana pasi moja ya bao kati ya 33 ambayo yamefungwa na timu hiyo.

Said Ntibanzokiza

Wamanuita ‘Father’ wa Yanga akiwa ni kiungo mwenye uzoefu mkubwa na soka la ushindani na amecheza mechi 12 katupia mabao 6 na ana pasi nne za mabao kayeyusha dk  1,048.

Feisal Salum

Mechi 16 kacheza ndani ya Yanga akiwa ameyeyusha dk 1,325 katupia mabao 4 na pasi 3 za mabao,kazi kubwa ni kwenye kutibua mipango ya wapinzani na kutengeneza nafasi.



Fiston Mayele

Namba moja kwa utupiaji akiwa na mabao 11 na pasi 3 za mabao. Kacheza mechi 19 na kusepa na dk 1,475.

Djuma Shaban

Mechi zake ni 16 na amefunga mabao 3 na pasi 3 huku akiwa kasepa na dk 1,437.

Simba

Aishi Manula

Air Manula kwenye himaya yake kaka langoni kwenye mechi 16 kafungwa mabao 7 akiwa naclean sheet 9 na n idk 1,440 kazitumia uwanjani.

Mechi yake ya kwanza kufungwa ilikuwa dhidi ya Ruvu Shooting na ni Elias Maguli alimuachia ganzi kwenye mikono yake kwa msimu wa 2021/22.

Henock Inonga

Kazi chafu zinaanza hapa kwenye eneo la kati katika mechi 13 ambazo kacheza ni dk 1,055 huku akiwa sio mtu mzuri ikiwa utamzingua kwa kuwa kutembeza vichwa kwake sio jambo gumu japo sio mchezo wa kiungwana kama alivyofanya mbele ya Coastal Union na kuonyeshwa kadi nyekundu ya moja kwa moja.

Sadio Kanoute

Mtaalamu wa mipira mirefu na mguso wake ni mara moja tu.Kiungo huyo amecheza jumla ya mechi 8 na kusepa na dk 668.

Katupia bao moja kwa kutumia kichwa akiwa ndani ya 18 na bado hajatoa pasi ya bao.

Bernard Morrison

Mzee wa kuchetua katumia dk 645 na amefunga bao moja na kutoa pasi mbili za mabao akiwapa washkaji zake Meddie Kagere na Mzamiru Yassin akiwa amecheza mechi 11.

Shomari Kapombe

Ili ukuta wa Pablo ukamilike utamkuta Kapombe mwenye pasi mbili na kutumia dk 1,24.

Meddie Kagere

Kwenye upande wa ushambuliaji kifaru hiki kutoka Rwanda ni namba moja na kimetupia mabao 7 na pasi moja ya bao.

Jonas Mkude

Mkongwe mwenye ujuzi mkubwa akiwa yupo kwenye ubora uleule kwa muda wa zaidi ya miaka 10, mpe kazi ya kucheza na mpira lazima utakubali kazi yake akiwa ametoa pasi mbili za mabao.


No comments:

Post a Comment

Post Top Ad