NASREDDINE Nabi, Kocha Mkuu wa Yanga amesema kuwa wanahitaji pointi tatu kwenye mechi zao zote ikiwa ni pamoja na ile dhidi ya Simba.
Yanga inaongoza ligi ikiwa na pointi 54 baada ya kucheza mechi 20 inatarajiwa kumenyana na Simba, Aprili 30, Uwanja wa Mkapa.
Nabi amesema kuwa mechi zao zote ambazo wanacheza ni muhimu na kila timu inahitaji pointi tatu hivyo wanajipanga kwa ajili ya mechi zote.
“Iwe tunakutana na Azam FC ama Simba ambacho tunahitaji ni pointi tatu, maana hizi mechi za dabi huwa zinakuwa na ushindani mkubwa lakini malengo yetu ni ushindi.
“Hakuna mechi ndogo kwetu wachezaji wanajua na kufikia lengo la kutwaa ubingwa ni lazima ushinde na kupata pointi kwenye mechi, hivyo tupo tayari kwa ushindani,” amesema Nabi.
Nabi atakuwa jukwaani kwenye mchezo ujao dhidi ya Simba unaotarajiwa kuchezwa Aprili 30 kutokana na kutumikia adhabu ya kadi nyekundu aliyoonyeshwa kwenye mchezo dhidi ya Geita Gold.
No comments:
Post a Comment