LIKIWEKWA tuta,asilimia 98 wengi wanahesabu ngoma lazima ijae wavuni lakini kuna mastaa wengi ambao wamekwama kufanya hivyo kwenye uwanja.
Kitete
cha kutetema hakikuwa kwa Fiston Mayele tu msimu huu hata Meddie Kagere wa
Simba alipata kitete cha kufunga.
Rekodi zinaonyesha kwamba kitete cha penalti kipo kwa mastaa wa Simba ambao
wamekosa penalti nyingi,hapa Championi Jumamosi linakuletea baadhi ya mastaa ambao walikosa kwenye ligi namna hii:-
Mastaa watano kutoka Simba
Mastaa
watano ndani ya kikosi cha Simba walikwama kufunga penalti ikiwa ni pamoja na
Rally Bwalya mbele ya Azam FC, John Bocco mbele ya Biashara United, Erasto
Nyoni mbele ya Ruvu Shooting, Chris Mugalu alikosa mbele ya Mbeya City na
Meddie Kagere alikosa mbele ya Biashara United.
Lakini
ikumbukwe kwamba Kagere ndani ya dakika 90 aliwahi kufunga kwa mkwaju wa
penalti mbele ya Tanzania Prisons kwenye mchezo uliochezwa Uwanja wa Mkapa na
Bwalya aliwahi kufunga mbele ya Polisi Tanzania.
Hivyo
kwa msimu huu wa 2021/22 mastaa wa Simba wamekuwa kwenye kigugumizi katika
kujaza kimiani penalti ambazo wanazipata ndani ya uwanja.
Pablo
Franco,Kocha Mkuu wa Simba aliliambia Championi Jumamosi kuwa huwa inatokea
wachezaji kushindwa kutumia mipira ya mapigo huru jambo ambalo linafanyiwa
kazi.
Mayele
Mei
9,2022 wakati ubao wa Uwanja wa Mkapa unasoma Yanga 0-0 Prisons itakuwa kwenye
kichwa cha Fiston Mayele pamoja na mashabiki wa Yanga ambao walikuwa wanaamini
kwamba atafikisha bao la 13 ila alikwama kumtungua Hussein Abel.
Penalti
iliyosababishwa na Feisal Salum baada ya kuchezewa faulo ndani ya 18 dk ya 37
na jukumu la penalti likawa miguuni mwa Mayele yeye alikosa.
Inakuwa
ni penalti ya kwanza kwake msimu huu kwenye ligi kukosa kwa kuwa katika mabao
yake 12 aliyonayo hajafunga kwa penalti.
Nasreddine
Nabi,Kocha Mkuu wa Yanga alisema kuwa Mayele hakupanga kukosa penalti hiyo ila
ilitokea kama ambavyo huwa inatokea kwa wachezaji wengine.
Boban na Masota
Oktoba
16,2021 ilikuwa ni siku ya makipa kuonyesha uwezo wao wa kuokoa penalti,ambapo
Uwanja wa Nyankumbu ulisoma Geita Gold 1-1 Mtibwa Sugar.
Kila
timu ilipata nafasi ya penalti ni Mtibwa Sugar walianza kupata dk ya 29
ikakoswa na Boban Zirintusa baada ya kipa Benedickt Tinocco kuweza kuokoa.
Pia
Geita Gold nao walipata penalti na mpigaji alikuwa ni Raymond Masota mikono ya
Aboutwalib Mshery ambaye kwa sasa yupo Yanga aliweza kuipangua penalti hiyo.
Mwaikenda
Lusajo
Mwaikenda wa Azam FC hakuwa na bahati ya kufunga ilikuwa mbele ya Geita Gold na
msababishaji wa penalti hiyo alikuwa ni kiungo mshambuliaji Idd Seleman,’Nado’.
Ilikuwa
ni Novemba 2,2021 Uwanja wa Azam Complex penalti hiyo iliokolewa na mikono ya
Khomeny Aboubakar ila Azam FC ilishinda bao 1-0.
Ambokile
Staa
wa Mbeya City,Eliud Ambokile hakuwa na bahati ya kufunga penalti ilikuwa mbele
ya Mbeya Kwanza kwenye mchezo wa ligi uliochezwa Uwanja wa Sokoine.
Ubao
uliweza kusoma Mbeya City2-2 Mbeya Kwanza na kipa wa Mbeya Kwanza aliyeweza
kupangua penalti hiyo anaitwa Hamad Juma.
Kisase
Anaitwa
Renatus Kisase wa Ruvu Shooting alikosa penalti mbele ya Mbeya City mchezo
uliochezwa Uwanja wa Sokoine ilikuwa ni Januari 20,2022 na ubao ulisoma Mbeya
City 1-0 Ruvu Shooting.
No comments:
Post a Comment