BAADA ya msoto wa kuambulia sare kwenye mechi tatu mfululizo,wachezaji wa kikosi cha Yanga kinachonolewa na Kocha Mkuu, Nasreddine Nabi wameweka wazi kwamba hawajapenda kupata sare.
Yanga ilianza
kuambulia sare mbele ya Simba ilikuwa Aprili 30 kisha ngoma ikawa Ruvu Shooting
0-0 Yanga na kigogo cha tatu ilikuwa ni Yanga 0-0 Tanzania Prisons.
Aboutwalib Mshery,kipa
namba mbili wa Yanga alisema kuwa matokeo ambayo wameyapata kwenye mechi
zilizopita hawajapenda hivyo watapambana kushinda mechi zijazo.
“Kupata sare sisi
hatujapenda lakini kwa kuwa ni matokeo basi tutazidi kupambana kwa mechi zijazo
ili kuweza kushindwa kwani mechi bado zipo na tunaamini kwamba tutashinda,”.
Mkongwe Deus Kaseke
alisema:”Tumepata sare mechi zilizopita hilo lishapita sasa tunaangalia mbele
kwa ajili ya kupata pointi tatu kazi bado haijaisha na tutazidi kupambana,”.
Dickson Ambundo winga
wa Yanga alisema;”Akili zetu ni kwa mechi zetu zijazo, sare zimeupa somo kuweza
kufanya vizuri kwa mechi zijazo lakini hayakuwa malengo yetu,” alisema.
Leo,Yanga inatarajiwa
kumenyana na Dodoma Jiji kwenye mchezo wa ligi unaoatarajiwa kuchezwa Uwanja wa
Jamhuri,Dodoma.
No comments:
Post a Comment