SIMBA NGOMA NZITO WATOSHANA NGUVU NA KMC - Dizo Click

Dizo Click

Hot

Post Top Ad

Wednesday, 7 September 2022

SIMBA NGOMA NZITO WATOSHANA NGUVU NA KMC

 


MOSES Phiri alitumia dakika mbili kufunga bao la kuongoza kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya KMC uliochezwa Uwanja wa Mkapa.

Dakika 90 zilikamilika kwa ubao wa Uwanja wa Mkapa kusoma Simba 2-2 KMC na kuwafanya wagawane pointi  mojamoja.

Kwa KMC, kipindi cha kwanza walikamilisha dakika 45 bila kufunga bao jambo lililowafanya warudi kivingine kipindi cha pili.

Matheo Anthony alipachika bao la kusawazisha dakika ya 48 na lile la pili kwa KMC lilifungwa na George Makang'a dakika ya 57.

Makosa ya safu ya ulinzi kwa Simba yalifanya mabao yote hayo yaweze kujazwa kimiani huku Simba wao wakiweka usawa kupitia kwa Habib Kyombo.

Ni bao la kwanza kwa Kyombo kufunga ndani ya Simba akitokea Mbeya Kwanza jambo lililowapa matokeo.


No comments:

Post a Comment

Post Top Ad