UBAO wa Uwanja Highland Estate dakika 45 unasoma Ihefu 1-1 Yanga ambapo kila timu imepata bao moja ambalo linawapeleka kwenye mapumziko.
Ni Yanga walianza kupata bao kupitia kwa Yannick Bangala ambaye alipachika bao kwa kichwa akitumia pasi ya Lomalisa.
Kwa upande wa Ihefu bao lao lilipatikana kupitia kwa Tigere ambaye alipiga pigo la faulo lilimshinda kipa namba moja Diarra Djigui.
Bangala alipachika bao hilo dakika ya 8 na lile la kuweka usawa kwa Ihefu ni mali ya Tigere dakika ya 43.

No comments:
Post a Comment