MATAIFA matatu yalifanya kazi kubwa kuipaisha Yanga kimataifa na kuipeleka kwenye hatua ya makundi Kombe la Shirikisho Afrika.
Ni kupitia bao pekee la ushindi la Aziz Ki raia wa Burkina Faso
ambaye alifunga bao hilo dakika ya 79 akitumia pasi ya Fiston Mayele raia wa DR
Congo.
Ikumbukwe kuwa kabla ya bao kupatikana lilipita kwenye miguu ya
wazawa wawili ambao ni Farid Mussa aliyemmegea pande Salim Aboubhakari aliyetoa
pasi kwa Mayele.
Kocha Msaidizi wa Yanga, Cedrick Kaze amesema kuwa kila mchezaji anatimiza majukumu yake kwa wakati kwa ajili ya
ushindi.
“Wachezaji wote wanatimiza majukumu ambayo wanapewa na
ushirikiano ni jambo kubwa linalofanyika kwa kila mchezaji hivyo ushindi kwetu
ni jambo linalotupa furaha,”.

No comments:
Post a Comment