MSHAMBULIAJI wa Yanga, Fiston Mayele kayeyusha jumla ya dakika 280 uwanjani bila kufunga kwenye mechi za Ligi Kuu Bara msimu wa 2022/23.
Nyota huyo kibindoni katupia mabao matatu na mara ya mwisho kufunga ilikuwa kwenye mchezo wa ligi dhidi ya Mtibwa Sugar alipofunga bao dakika ya 38, Uwanja wa Mkapa.
Mechi nne zilizofuata nyota huyo kakwama kufunga ilikuwa dhidi ya Ruvu Shooting alipoyeyusha dakika 90, Simba dakika 90 Geita Gold alisepa na dakika 16 na mchezo dhidi ya Kagera Sugar aliposepa na dakika 90.
Ikumbukwe kwamba msimu wa 2021/22 nyota huyo alifunga mabao 16 na kuwa mtupiaji namba mbili ambapo mtupiaji namba moja alikuwa ni George Mpole wa Geita Gold ambaye msimu huu amekuwa mpole kwenye suala la kucheka na nyavu.
Kesho Yanga ina kibarua cha kusaka ushindi mbele ya Singida Big Stars mchezo unaotarajiwa kuchezwa Uwanja wa Mkapa.

No comments:
Post a Comment