NAMUNGO KAMILI KUIKABILI SIMBA - Dizo Click

Dizo Click

Hot

Post Top Ad

Tuesday, 15 November 2022

NAMUNGO KAMILI KUIKABILI SIMBA

 


KOCHA msaidizi wa Namungo, Shadrack sajigwa amebainisha kuwa wachezaji wote wapo kamili kwa ajili ya kuikabili Simba.


Kikosi cha Namungo kimeshatia timu ndani ya Dar ambapo kilifanya maandalizi ya mwisho Ruangwa,Novemba 13 kabla ya kuibukia kwenye jiji la Biashara.


Miongoni mwa nyota ambao wapo kwenye kikosi hicho ni pamoja na Shiza Kichuya ambaye aliwahi kucheza Mtibwa Sugar na Simba kwa mafanikio pia mtupiaji wao namba moja ni Relliats Lusajo mwenye mabao sita.


Nsajigwa amesema:"Tupo tayari kwa ajili ya kuikabili Simba na tunahitaji pointi tatu na hatuna mchezaji majeruhi,".

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad