SABABU ZA MATOLA KUCHELEWA KUSOMA HIZI HAPA - Dizo Click

Dizo Click

Hot

Post Top Ad

Wednesday, 23 November 2022

SABABU ZA MATOLA KUCHELEWA KUSOMA HIZI HAPA

 


SELEMAN Matola, Kocha Msaidizi wa Simba amesema kuwa sababu kubwa ya yeye kuchelewa kusoma kozi ya ukocha Leseni A ya CAF anayoisomea kwa sasa ni upatikanaji wa nafasi hizo.


Matola kwa sasa yupo masomoni akiendeleza ujuzi wake wa masuala ya ufundishaji ambapo gharama za malipo zinasimamiwa na waajiri wake Simba.


Kocha huyo amesema:"Hizi kozi huwa haziji mara nyingi kwenye hatua hii wakati wmingine huwa inachukua miaka mingi na kwa kuwa imekuja kwa wakati huu acha niendelee kusoma kwa kuwa hakuna mtu ambaye hapendi kufikia mafanikio anayohitaji,".


Mbali na Matola pia yupo kocha msaidizi wa Ihefu, Zuber Katwila ambao wapo kwenye kozi ya ukocha ya CAF A Diploma wakiendelea na mafunzo visiwani Zanzibar na kuna washiriki 25 kutoka Tanzania, Zambia, Zimbabwe, Rwanda na Somalia wapo pia.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad