TIMU ya taifa ya Senegal kutoka Afrika imeushangaza ulimwengu kwa kuitungua Ecoadar mabao 2-1 na kutinga hatua ya 16 bora Kombe la Dunia, Qatar 2022.
Mchezo huo wa hatua ya makundi ulikuwa na ushindani mkubwa ambapo Senegal walikuwa wanapewa nafasi kubwa ya kushinda mchezo huo.
Bao la mapema lilifungwa na staa Ismaila Sarr dakika ya 44 kwa mkwaju wa penalti na lilidumu mpaka muda wa mapumziko ilikuwa ni Novemba 29,2022.
Mzani uliwekwa sawa dakika ya 67 na Moises Caicedo kisha dakika tatu mbele staa wa Senegal, Kalidou Koulibaly alipachika bao la ushindi.
Mbele ya mashabiki 44,569 waliojitokeza Uwanja wa taifa wa Khalifa walishuhudia soka safi kutoka kwa Waafrika waliokuwa wakipambana mwanzo mwisho bila kuchoka.
Baada ya kutinga hatua ya 16 bora mchezo wao ujao watakutana na England kwenye hatua ya 16 ya Kombe la Dunia unatarajiwa kuchezwa Desemba 4,2022.
Kutoka kundi A, Senegal inamaliza ikiwa nafasi ya pili na pointi zake ni 6 huku kinara akiwa ni Netherlands mwenye pointi 7.
Ecoador nafasi ya tatu kwenye msimamo wana pointi nne na wenyeji Qatar hawa waliaga mashindano mapema wapo nafasi ya tatu hawajakusanya pointi hata moja.

No comments:
Post a Comment