YANGA KUFANYA MABORESHO KIKOSI KAZI - Dizo Click

Dizo Click

Hot

Post Top Ad

Monday, 21 November 2022

YANGA KUFANYA MABORESHO KIKOSI KAZI


 MIONGONI mwa sehemu ambazo inaelezwa kuwa Kocha Mkuu wa Yanga Nasreddine Nabi anahitaji kufanya maboresho ni kwenye safu ya ulinzi.


Nabi anatajwa kuhitaji kuongeza beki mmoja wa kazi ambaye atawaongezea ushindani Dickson Job na Kibwana Shomari.

Pia kwa upande wa kiungo anatajwa kusaka mmoja ili kuongeza nguvu kwenye kikosi hicho kuelekea kwenye dirisha dogo la usajili linalotarajiwa kufunguliwa Desemba 15.

Kikosi cha Yanga kwa sasa kipo Singida kwa ajili ya maandalizi ya mwisho ya mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Dodoma Jiji unaotarajiwa kuchezwa kesho Novemba 22, Uwanja wa Liti.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad