BEKI WA KAZI KAMILI YANGA - Dizo Click

Dizo Click

Hot

Post Top Ad

Monday, 5 December 2022

BEKI WA KAZI KAMILI YANGA


UONGOZI wa Yanga umeweka wazi kuwa beki wao wa kazi ngumu Djuma Shaban hali yake kwa sasa inaendelea vema baada ya kupata maumivu hivi karibuni.

Djuma hakuwa sehemu ya kikosi kilichopoteza kwa kufungwa mabao 2-1 dhidi ya Ihefu mchezo uliochezwa Uwanja wa Highland Estate ambapo rekodi ya Yanga kutofungwa mechi 49 iligotea hapo mazima.

Ofisa Habari wa Yanga, Ally Kamwe amesema kuwa maendeleo ya nyota huyo kwa sasa yanaendelea vizuri kwa mujibu wa ripoti za madaktari.

“Hali ya Djuma kwa sasa inaendelea vizuri jambo ambalo tunamshukuru Mungu kwa hili na tunaamini kwamba atarejea uwanjani kuendelea na majukumu yae.

“Hata Farid Mussa naye hakuwepo kutokana na kuwa na matatizo ya kifamilia.Kuhusu mipango yetu kila kitu kinakwenda sawa na tunaamini kwa mechi zetu tutapata matokeo chanya,”.

Djuma ni mechi 8 kacheza akiyeyusha dakika 520 kafunga bao moja na pasi moja ya bao alikuwa sehemu ya kikosi kilichoshinda bao 1-0 dhidi ya Tanzania Prisons, Uwanja wa Mkapa.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad