HII HAPA RATIBA YA SIMBA KIMATAIFA - Dizo Click

Dizo Click

Hot

Post Top Ad

Tuesday, 13 December 2022

HII HAPA RATIBA YA SIMBA KIMATAIFA

 


WAWAKILISHI wa Tanzania, Simba kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika hatua ya makundi wamedondokea kundi C.


Droo ilichezeshwa nchini Misri Desemba 12,2022 ambapo kila mmoja amejua mpinzani wake atakuwa ni nani.

Katika makundi hayo Simba ipo pamoja na timu za Raja Casablanca, Horoya na Vipers ya kutoka Uganda.

Ratiba ya Simba kimataifa inatarajiwa kuwa namna hii:-Feb 10 itakuwa ni Horoya v Simba ambapo itakuwa ugenini kisha Feb 17 itakuwa ni Simba v Raja na kigongo chao kijacho itakuwa ni Feb 24 dhidi ya Vipers pia hapa Simba atakuwa ugenini.


Machi 7,2023 ni Simba v Vipers, Machi 17 ni Simba v Horoya na Machi 31 ni Raja v Simba.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad