KIPA YANGA HATIHATI KUIVAA POLISI TANZANIA - Dizo Click

Dizo Click

Hot

Post Top Ad

Saturday, 17 December 2022

KIPA YANGA HATIHATI KUIVAA POLISI TANZANIA


 KIPA namba mbili wa Yanga, Aboutwalib Mshery leo kuna hatihati ya kuwavaa wapinzani wao Polisi Tanzania kwenye mchezo wa ligi unaotarajiwa kuchezwa Uwanja wa Mkapa.

Yanga ikiwa nafasi ya kwanza na pointi 38 inatarajiwa  kumenyana na Polisi Tanzania iliyo nafasi ya 16, Uwanja wa Mkapa.

Cedrick Kaze, kocha msaidizi wa Yanga amesema kuwa maandalizi yapo tayari na wapo wachezaji ambao watakosekana kutokana na sababu mbalimbali.  

“Mshery, (Aboutwalib) bado hajarejea kwenye ubora wake na kwa upande wa mchezaji mmojammoja maangalizi ya mazoezi ya mwisho yataamua nani atakuwa tayari kwa ajili ya mchezo wetu.  

“Itakuwa ni mechi ya tofauti dhidi ya Polisi Tanzania, tumeona timu imebadilika kwenye mechi za mwisho na tuliona ilicheza na Azam FC, kwa muda mrefu tutakuwa kwenye hali nzuri kwa kuwa wachezaji wengi wanaweza kupata nafasi kwa kuwa wote wanaweza kushiriki,” amesema Kaze.

Kocha msaidizi wa Polisi Tanzania, John Tamba amesema kuwa makosa ambayo walifanya mzunguko wa kwanza wamefanyia kazi.

“Hatukuwa na mzunguko wa kwanza mzuri, makosa yetu tumefanyia kazi na tuna amini tutapata matokeo kwenye mchezo wetu kwa kwa maandalizi yapo sawa,”.

Jeremia Juma kipa wa Polisi Tanzania amesema kuwa wanatambua mchezo utakuwa mgumu lakini wanahitaji ushindi.

“Tutashinda mchezo wetu, mashabiki ambao hawakuwa na mpango wa kuja uwanjani waje kwa kuwa wachezaji tupo tayari na tunaamini tutapata matokeo,”.

 

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad