UNAONA namna ushindani ndani ya Kombe la Dunia na kila timu inafanya kweli kupata matokeo baada ya dakika 90 kukamilika?
Hakika
kuna jambo ambalo lipo kwenye mashindano haya makubwa na kila mmoja anafanya
kazi yake kutimiza majukumu yae.
Umependa
namna Korea Kusini inavyocheza kukamilisha dakika 90 kwenye mchezo wao mmoja
wakiwa hawana mambo mengi ndani ya uwanja?
Hujapenda
kuwaona Wajapan wakisaka mpira katika Kombe la Dunia huko Qatar 2022, bado
hujapata jambo hapo kutokana na kasi yao licha ya kugotea njiani?
Kwenye vichwa vyao akilini mwao neno kushindwa halipo hata kama wanakutana na ugumu kiasi
gani hasa wanapohitaji kufikia mafanikio ambayo wanahitaji.
Muda
ni sasa wa kujifunza kutokana na kile ambacho wanakifanya kutoka huko mbele na
sasa kuhamia kwenye akili zetu katika utendaji.
Umeona
makosa ambayo wachezaji wetu kutoka Afrika wanafanya namna ambavyo yanafanana
kwenye kila mchezo?
Unadhani
kwa nini inakuwa hivyo kwetu kila siku, wale unaowapa nafasi ya kufanya vizuri
wanazingua na wale ambao huwatarajii wanakupa kitu ambacho hukitarajii, lazima
kuwe na mabadiliko wakati ujao.
Ghana,
unadhani walikuwa wamekosa nini mpaka kugotea kwenye nafasi ya makundi Kombe la
Dunia Qatar licha ya kuwa kwenye mwendo mzuri, kuna la kujifunza pia.
Cameroon mchezo mzuri walioonyesha mbele ya Brazil na kupata ushindi mwanzo walikuwa wamekwenda wapi ama walidhani kwamba wapo peke yao kwenye mashindano hayo?
Yote
kwa yote timu kutoka Afrika zimeonyesha namna ambavyo zinaweza kuwapa kitu
mashabiki na kufanya kweli kweye mechi zote.
Ukweli
ni kwamba kila wachezaji ambao wanapata nafasi kwenye mechi katika Kombe la
Dunia wanajitoa kwa asilimia 100 bila kujali aina ya timu ambayo inacheza.
Kwa
kila timu hapa tunaona kwamba malengo makubwa kwenye mechi ambayo wanacheza
wanakubaliana kucheza bila kuogopa na hili ni jambo la kujifunza.
Nina
amini kwamba wachezaji wazawa wanapata muda wa kutazama namna wapinzani
wanavyopata upinzani kwenye mechi ambazo wanacheza.
Hakuna
ambaye anakubali kuona anashindwa hata kama watakuwa wamepoteza mchezo kipindi
cha kwanza ama kipindi cha pili.
Muda
wote wanajipanga na kuanza upya kama hakuna kilichotkea na mashabiki wamekuwa
wakishangilia muda mwingi hili ni jambo lingine.
Kwa
maana hiyo mashabiki wana kitu cha kujifunza na wachezaji wana kitu cha kujifunza
kwenye hili Kombe la Dunia Qatar.
Wapo
ambao wamekwenda kutazama namna gani wengine wanacheza na wengine wamekwenda
kutazama mpira na mazingira.
Muda
mzuri wa kujifunza kwa wakati mwingine kwenye mechi zijazo ikiwa wameshindwa na
wale ambao watakuwa na muda wa kujipanga kwa mechi zijazo ni muhimu kuendelea
kufanya kazi nzuri.
Hakika
ukweli ni kwamba ushindani ni mkubwa na unavutia kwa kila timu kuingia uwanjani
kusaka ushindi na hili linaleta kitu kizuri.
Wachezaji
mmeona namna wachezaji wengine ambao wanafanya kazi kutafuta ushindi bila
kukata tamaa na mwisho matokeo yanapatikana.
Pongezi
kwa wale ambao wanajifunza jambo kupitia Kombe la Dunia iwe hivyo hata
watakapokuwa kwenye mechi zao za ushindani uwanjani.
Kila
kitu kinawezekana kutokana na mipango ambayo inapangwa ndani ya dakika 90
hakuna kazi nyepesi kwenye kusaka ushindi.
Iwe
unashabikia Ghana, Cameroon, Morocco ama Brazili au mabingwa watetezi Ufaransa
ninaona mmeona namna ushindani ulivyo.
Hapa
hakuna timu yenye uhakika asilimia 100 kusepa na ubingwa kutokana na namna
ambavyo wapinzani wanafanya maandalizi yao.
Hakika
ni wakati mzuri wa kujifunza na kufanya vizuri kwa wakati ujao.
No comments:
Post a Comment