MESSI AKIWASHA WAKITINGA FAINALI KOMBE LA DUNIA - Dizo Click

Dizo Click

Hot

Post Top Ad

Wednesday, 14 December 2022

MESSI AKIWASHA WAKITINGA FAINALI KOMBE LA DUNIA

 


NAHODHA wa Timu ya Taifa ya Argentina, Lionel Messi amefanikiwa kuandika rekodi nyingine kufika na timu hiyo mara mbili kwenye hatua ya fainali ya Kombe la Dunia.

Ushindi wa mabao 3-0 waliopata mbele ya Croatia kwenye mchezo wa nusu fainali ya kwanza iliyochezwa Uwanja wa Lusail Iconic umewapa tiketi hiyo Argentina.

Ilikuwa mbele ya mashabiki 88,966 ambao walijitokeza uwanjani kuhsuhudia mchezo huo uliokuwa na ushindani mkubwa.

Ni muungano wa mastaa wawili wa Argentina ulihusika kwenye mabao hayo matatu ikiwa ni yeye mwenyewe Messi pamoja na Julian Alvarez.

Messi alifungua pazia la ufungaji ambapo alipachika bao dakika ya 34 kisha Alvarez alipachika mawili dakika ya 39 na 69.

Sasa Messi atakutana na mshindi kati ya mchezo wa Morroco dhidi ya mabingwa watetezi Ufaransa ambao unatarajiwa kuchezwa leo.

Mara ya mwisho kwa Argentina kutinga hatua ya fainali Kombe la Dunia ilikuwa 2014 na illipoteza kwa kufungwa bao 1-0 dhidi ya Ujerumani.

Pia haijatwaa taji hilo kubwa duniani tangu mwaka 1986 zama za Diego Maradona ambaye aliongoza taifa hilo kutwaa taji hilo Mexico.

Messi amesema kuwa walikuwa wamechoka kutokana na kucheza mechi ngumu lakini hawakuwa na namna walipambana kupata ushindi.

"Tulikuwa tumechoka kutokana na mechi za ushindani lakini tulikubaliana kufanya vizuri na kupata matokeo. Unajua mchezo wetu tuliofungwa na Saudi Arabia ulikuwa ni mgumu kwetu kwa kuwa tulikuwa hatujafungwa kwenye mechi sita.

"Kuanza vile kama ambavyo tulikuwa tumeanza hatukufikiria kama tungeweza kufungwa lakini ilikuwa ni chachu kwetu na tukaamua kuonyesha tunaweza kiasi gani kuwa kwenye ushindani na kila mechi kwetu ilikuwa ni fainali,".

Kocha Mkuu wa Croatia. Zlatko Dalic amesema kuwa inawezekana ikawa ni mwisho wa kizazi cha kombe la dunia kutokana na umri wa wachezaji.

Miongoni mwa wachezaji ambao hawatakuwa kwenye kikosi hicho wakati ujao ni Luka Modric mwenye miaka 37 ambaye hili ilikuwa ni mara yake ya mwisho kushiriki Kombe la Dunia.

"Nadhani itakuwa ni mwisho wa kizazi chetu kwenye Kombe la Dunia, wengi wamefikia umri wao lakini tusubiri na kuona itakuaje 2026.

"Lakini kizazi hiki kitakwenda kushiriki Euro 2024 nadhani hapo kitakuwa kimegotea mwisho na tulikuwa na kizazi kizuri ambacho kimefanya vizuri kwenye timu ya taifa na mkataba wangu utaisha 2024.

"Kuhusu Messi ni mchezaji bora na tulitarajia kwamba tungeona yale ambayo ameyafanya,".



No comments:

Post a Comment

Post Top Ad