NYOTA Lionel Messi aliiongoza Argentina kutwaa
ubingwa wa Kombe la Dunia kwa kuwashinda mabingwa watetezi Ufaransa kwa mikwaju
ya penalti 4-2 baada ya sare ya 3-3 ndani ya dakika 120.
Katika mchezo huo ambao utaingia kwenye
historia ya kuwa miongoni mwa mchezo mkubwa wa fainali kupata kuchezwa kwa
vigogo hao wawili Uwanja wa Lusail Iconic.
Ufaransa
walitoka nyuma mara mbili wakipindua meza jambo lililofanya mchezo huo mshindi
kupatikana kwa mikwaju ya penalti.
Licha ya kwamba Messi atachukuwa vichwa vya
habari, Kylian Mbappe alikuwa mchezaji wa kwanza kufunga hat-trick kwenye
fainali ya Kombe la Dunia tangu Sir Geoff Hurst akiwa na England kufanya hivyo mwaka 1966.
Argentina walitawala kwa dakika 80 za
mwanzo na walionekana kujiandaa kunyakua taji lao la kwanza la Kombe la Dunia
tangu 1986. Messi aliifungia timu yake mkwaju wa penalti dakika ya 23 baada ya
Ousmane Dembele kuhukumiwa kumkwaa Angel Di Maria.
Winga wa Juventus Di Maria aliiongezea
Argentina bao la pili baada ya kuwa kwenye spidi kwa kuongozwa na pasi elekezi
ya Alexis Mac Allister wa Brighton huku
Ufaransa ikionekana kukabiliwa na madhara ya ugonjwa kambini.
Ni dakika ya 79 baada ya Randal Kolo Muani
kuangushwa na Nicolas Otamendi Mbappe alifunga bao lake la kwanza jioni, kabla
ya kuongeza la pili sekunde 90 baadaye na kupeleka mchezo kwenye muda wa ziada.
Mbappe alifunga bao la kwanza dakika ya 80
na lile la pili dakika ya 81 ikiwa ni muda mfupi wa kutengenanisha ubingwa kwa
mchezaji mwenzake anayecheza naye PSG Messi.
Messi alidhani ameshinda kwa upande wake
huku bao lake la pili lilitolewa na teknolojia ya mstari wa goli katika dakika
ya 108. Lakini, zikiwa zimesalia dakika chache za mchezo, Ufaransa walipata
penalti nyingine baada ya Gonzalo Montiel kuonekana akishika mpira kwa mkono
kwenye harakati za kuokoa.
Mbappe aliongeza kwa mara ya pili na kwa
mara nyingine kumpiga Emiliano Martinez, na kuwafanya Ufaransa kurejea kwenye
sare kwa mara ya pili na kupeleka mchezo kwenye mikwaju ya penalti.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 23
alifunga bao lake la tatu jioni kabla ya
Messi kujibu.
Lakini Kinsgley Coman na Aurelien
Tchouameni wote walikosa mikwaju yao ya penalti kwa Ufaransa huku Argentina
ikifunga kila moja kati ya matatu yaliyosalia, huku Montiel akipiga mkwaju wa
penalti wa ushindi na kushinda Kombe la Dunia la 2022.

No comments:
Post a Comment