RASMI nyota wa kikosi cha Geita Gold George Mpole msimu huu hatakuwa kwenye kikosi hicho baada ya uongozi kutihibitisha kuwa umeaachana naye.
Mpole alikuwa kwenye mvutano na mabosi wake hao mwanzoni mwa msimu huu jambo ambalo ilipelekea awe nje kwa muda na alirejea hivi karibuni na kuanza mazoezi na timu hiyo inayoshiriki Ligi Kuu Bara.
Klabu ya Soka ya Geita Gold imetangaza kuachana na nyota wake anayeshilia tuzo ya ufungaji bora msimu uliopita wa 2021/22 kwenye NBC Premier League kwa makubaliano ya pande zote mbili.
Taarifa hivyo iliyotolewa na Geota Gold imeeleza:-“Uongozi umefikia hatua hii baada ya kuzungumza na mchezaji kwa kina na kufikia maridhiano hayo kwa maslahi mapana ya klabu na mchezaji mwenyewe” sehemu ya taarifa ya klabu hiyo iliyowekwa kwenye ukurasa wao wa Instagram.
Kwenye msimu uliopita wa 2021/22 Mpole alitupia 17 na kutoa pasi za mwisho (assist) nne.

No comments:
Post a Comment