UONGOZI wa Mtibwa Sugar umesema kuwa kwa sasa unasubiri ripoti ya benchi la ufundi ili kufanikisha mpango wa kusajili wachezaji wapya.
Dirisha dogo la usajili linatarajiwa kufunguliwa wiki ijayo ambapo timu hupewa muda wa kuboresha nafasi ambazo wataona zinahitaji kuongezewa nguvu.
Miongoni mwa wanaosakwa ndani ya Mtibwa Sugar ni kwenye eneo la ushambuliaji pamoja na ulinzi.
Ofisa
Habari wa Mtibwa Sugar, Thobias Kifaru amesema kuwa baada ya kumalizana na
Geita Gold wamerejea na sasa wanaanza kujipanga upya.
“Mchezo wetu wa mwisho mzunguko
wa kwanza tumemaliza dhidi ya Geita Gold ugenini na kupata sare ya kufungana
mabao 2-2 hivyo kwa sasa tunasuiri ripoti ya benchi la ufundi kuifanyia kazi.
“Tumekusanya pointi 22 baada ya
kucheza mechi 15 tukiwa kwenye nafasi ya sita hivyo kuna jambo ambalo tumeona,
tukipata ripoti ya benchi la ufundi tutaona nini wamependekeza tufayie kwa
ajili ya mzunguko wa pili.
“Mapendekezo ya mwalimu ambayo
yatatolewa hayo tutafanyia kazi kwa ajili ya kuongeza nguvu kwenye kikosi chetu
kwa ajili ya mzunguko wa pili,”.

No comments:
Post a Comment