BAADA ya kuiongoza timu ya Taifa ya Ureno kwenye Kombe la Dunia 2022 Qatar na kutolewa katika hatua ya robo fainali na Timu ya Taifa ya Morocco, Fernando Santos aliyekuwa kocha mkuu wa timu hiyo amebagwa manyanga jumlajumla.
Baada ya kocha huyo kubwaga manyanga jina la kocha wa Roma, Jose Mourinho ni miongoni mwa jina linalotajwa kwa waliopendekezwa mapema kuchukua nafasi ya Santos.
Ikumbukwe kwamba kwenye mechi zake za mwisho Fernando Santos alichukua uamuzi mgumu kumuweka benchi Cristiano Ronaldo kwenye mchezo wa hatua ya makundi ya Kombe la Dunia.
Kwenye mchezo wao dhidi ya Uswisi hatua ya 16 bora alianza na Goncalo Ramos kikosi cha kwanza badala ya Ronaldo ambapo mbadala wake huyo alifunga hat-trick katika ushindi wa 6-1 dhidi ya Uswizi.
Ronaldo aliingia kama mchezaji wa akiba katika mechi ya robo fainali dhidi ya Morocco lakini hakuweza kuipa ushindi timu hiyo kwenye mchezo huo.
Santos mara kwa mara alikabiliwa na maswali kuhusu kumwacha Ronaldo, huku mshambuliaji huyo wa zamani wa Manchester United akikana ripoti iliyodai kuwa alitishia kuondoka Qatar kwa kutokuwa na mawasiliano mazuri na kocha wake.
Ureno sasa wataanza mchakato wa kumteua kocha mkuu mpya, huku kocha wa Roma Jose Mourinho akiwa mmoja wa watu wanaopewa nafasi hiyo mapema.
Taarifa ya Shirikisho la Soka la Ureno
ilisema: "Ilikuwa heshima kuwa na kocha na mtu kama Fernando Santos kwenye timu ya taifa.
"Bodi ya FPF sasa itaanza mchakato wa kuchagua kocha wa kitaifa ajaye."

No comments:
Post a Comment